

소개
Mzingile ni novela (riwaya fupi) ya kifalsafa na kibaadausasa iliyochapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1991. Riwaya hii ni pacha ya ile ya Nagona (1990). Riwaya hii inasawiri chimbuko, maendeleo, maangamizi na kuzaliwa upya kwa dunia kutokana na fujo za wanadamu.Kakulu, mhusika kiini wa novela hii, anasemekana kuwa alizaliwa kiajabuajabu, na umbo lake na maisha yake kwa jumla yalikuwa ni ya kushangaza na kutatanisha, yakihusishwa na matukio ya ajabu na uwezo usio wa kawaida aliosadikiwa kuwa nao.



