

소개
?Binti mfalme Zuwena ni kitinda mimba kati ya watoto watatu, anayeishi katika ufalme wa kisiwa cha Amani chenye shamrashamra nyingi. Tofauti na dada zake, yeye anachukia maisha ya ikulu yanayomnyima uhuru na anapendelea kuzurura masokoni akiwa ameficha utambulisho wake. Siku moja, anagundua kanga ya kale inayomeremeta ndani ya sanduku lililofichwa.?Punde si punde, anatambua kuwa methali zilizochapishwa kwenye pindo za kanga za kifalme si ushauri tu-bali ni maelekezo ya siri.



